Saturday, April 7

LAZIMA WAWEPO MADEREVA WAWILI KWA MABASI YAENDAYO MIKOANI-KAMANDA MWANGAMILO

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni kimesema mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi jirani lazima wawepo  madereva wawili na hilo haliepukiki.

Akizungumza na Michuzi Blog, leo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Solomon Mwangamilo amesema ukaguzi wa mabasi na madeva wawili ni endelevu katika kuhakikisha abiria wanasafiri salama.

Mwangamilo amesema wamiliki mabasi wahakikishe wanazingatia usalama wa mabasi na abiria.Pia wahakikishe kunakuwa na madereva wawili ambao watapokeza kuendesha wakiwa safarini.Amesema basi likitoka katika kituo cha Ubungo lazima madereva wawili wasaini na mpaka wanafika katika kituo chao mwisho wanahakikiwa, hivyo hakuna mtu anayeweza kufanya udanganyifu kutokana na mtando uliopo katika jeshi la Polisi.

Mwangamilo amesema wanaoingiza mabasi ambayo mabovu na kutegemea wataondoka na abiria kituo cha mabasi Ubungo wanajidanganya  na wataofanya hivyo watakwenda jela.“Kazi yetu ni kuhakikisha wananchi wanasafiri na mabasi yakiwa salama kutokana ukaguzi unaofanyika kila kukicha na hakuna basi litakaloachwa huku likiwa lina ubovu wa kuhatarisha watumiaji wa usafiri huo” amesema Mwangamilo.


Aidha amesema askari katika mkoa wa Kinondoni hasa kituo cha mabasi Ubungo kuwa kufanya kazi ya ukaguzi bila kikomo katika kuwalinda usalama wa abiria wanatumia mabasi ya mikoani na nchi jirani.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo , Nuru Hussein akimpa maelekezo dereva wakati wakifanya ukaguzi mabasi kutuo hicho, leo jijini Dar es Salaam.
Abiria wakishuka katika Basi la Princess Line linalofanya safari zake Dar es Salaam ,Babati baada ya Basi hilo kuonekana na hitilafu takiribani ya masaa manne katika kituo cha Ubungo na kufanya kampuni kuwabadilishia basi lingine.
Askari wa Usalama Barabani katika kituo kikuu cha Ubungo, Koplo Rashid Abdallah akizungumza na abiria walio kaa zaidi ya masaa manne katika Basi la Princess Line, leo .jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabasi yalikutwa na kamera yetu katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo

No comments:

Post a Comment