Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Michael Wambura ameamua kufunguka na kujibu hoja ambazo zimetolewa dhidi yake.
Wambura ameweka wazi kujibu hoja moja baada ya nyingine kuhusu rufaa iliyosomwa jana na Kamati Rufani ya Maadili ya TFF.
Rufaa ya Wambura ilitupiliwa mbali baada ya Kamati ya Rufaa kuona haina mashiko.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Wambura amesema yeye pamoja na jopo lake la Mawakili wanasubiri hukumu ya rufaa hiyo (Jumatatu) ili kuijadili kwa kina kuhakikisha rufaa inaendelea.
Amesema yaliyosomwa jana katika rufaa yake si yale yalioandikwa wakati wakupeleka rufaa hiyo.Amedai kuwa suala hilo lakisheria limetoka katika Mpira na badala yake linakwenda katika maisha yake binafsi.
Kuhusu Kesi ya Simba, Wambura amesema kuwa kesi hiyo ilifutwa tangu 13/4/2017, amesema haikuwa na mashiko mbele yake.Kwa upande wa Wakili wake, Emmanuel Muga amedai Kamati iliyotoa uamuzi ilibadirishwa kwa baadhi ya Wajumbe, amedai Kamati haikuwa halali.
No comments:
Post a Comment