Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar wameitembelea Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa lengo la kudumisha ushirikiano na kujifunza mbinu mbalimbali zinazotumiwa na Bodi katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii, Bw. Geofrey Meena alitoa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi ikiwa pamoja na namna inavyoshirikiana na Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali, Mabalozi wa Hiari wa Utalii wanavyosaidia kutangaza utalii wa Tanzania katika nchi zao, Namna Bodi inavyoshirikiana na vyombo mbalimbali vya Habari vya ndani na nje katika kutayarisha vipindi vya utalii wa Tanzania.
Aidha Bw, Meena alisisitiza kuwa mialiko ya Timu maarufu za mchezo wa mpira wa miguu kuwa moja ya njia yenye manufaa makubwa katika kuitangaza Tanzania
Ujumbe huo uliyongozwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma ambaye alionyesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Bodi, alisema “ziara yetu imekuwa ni ya mafanikio kwani tumeweza kujifunza mikakati inayotumiwa na Bodi katika kutekeleza jukumu lake la kutangaza utalii wa Tanzania hasa Utalii wa Ndani”.
Ujumbe huo uliyongozwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma ambaye alionyesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Bodi, alisema “ziara yetu imekuwa ni ya mafanikio kwani tumeweza kujifunza mikakati inayotumiwa na Bodi katika kutekeleza jukumu lake la kutangaza utalii wa Tanzania hasa Utalii wa Ndani”.
Pia ujumbe huo uliipongeza Bodi kwa kuwa na mipango madhubiti ya utangazaji pamoja na kutengeneza video maalumu inayotumika kuvitangaza vivutio hivyo katika matukio mbalimbali ya kimataifa. Ziara hiyo Ilifanyika tarehe 28/08/2017.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii, Bw. Geofrey Meena akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Baraza la wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utaliiya Zanzibar walipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii, Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Baraza Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar akitumia lugha ya alama kutafsiri jambo kwa moja ya mjumbe wa Baraza Hilo.
Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment