Tuesday, August 29

Israel: Iran inajenga kiwanda cha makombora Syria

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inatengeza kiwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.Haki miliki ya pichaALAMY
Image captionWaziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inatengeza kiwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inajenga viwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.
Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kwa kuifanya Syria kuwa kambi yake kutengeza vifaa vya kijeshi kama mpango wake wa kutaka kuiangamiza Israel.
Majeshi ya Iran yanamsaidia rais Bashar al Assad katika vita vya Syria huku ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Lebanon Hezbollah.
Matamshi ya Netanyahu yanajiri baada ya kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutierrez mjini Jerusalem.
Bwana Guterres amefanya ziara yake ya kwanza katika enewo hilo tangu kuchukua mamlaka mnamo mwezi januari.
Bwana Netanyahu hakutoa maelezo kuhusu viwanda hivyo vya Iran lakini akaonya kwamba hicho ''ni kitendo ambacho Israel haitakubali''.
Wiki mbili zilizopita, kampuni ya Israel Imgesat ilichapisha picha ilizosema zinathibitisha ripoti ya gazeti moja la upinzani nchini Syria kwamba kiwanda cha makombora kilikuwa kikijengwa kaskazini magharibi mwa Syria chini ya uangalizi wa Iran.
Picha zinazoonyesha kuwa Iran huenda inajenga viwanda vya kutengezea makombora nchini SyriaHaki miliki ya pichaIMAGESAT INTERNATIONAL NV/REUTERS
Image captionPicha zinazoonyesha kuwa Iran huenda inajenga viwanda vya kutengezea makombora nchini Syria
Imagesat International ilisema kuwa kiwanda hicho katika eneo la wadi Jahannam , karibu na mji wa Baniyas uliopo katika pwani ya Mediterania kinafanana na kile cha kutengeza makombora karibu na Tehran.
Hakujakuwa na tamko lolote kutoka kwa Iran inayotaka taifa hilo Wayahudi kuangamizwa.
Bwana Netanyahu pia alimshinikiza Guterrez kuhusu walinda amani wa UN nchini Lebanon ,Unifil , ambapo Israel inadai wameshindwa kuwazuia wapiganaji wa Hezbollah kujiongezea silaha tangu vita vya 2006.
Bwana Guterres aliahidi kufanya kila awezalo ili kuhakikisha kuwa Unifil inaafikia malengo yake .
Ninaelewa wasiwasi wa kiusalama wa Israel na narejelea kwamba wazo hilo ama lengo la kuangamiza Israel ni swala ambalo halitakubalika kwa maoni yango.
Mkataba wa Unifil unatarajiwa kuongezwa mwisho wa mwezi.

No comments:

Post a Comment