Tuesday, August 29

Mahiga aeleza Sadc ilivyojizatiti kukabili ugaidi

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, 
Dk Augustine Mahiga 
Tanga. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga amesema kikundi chochote cha kigaidi au kiharamia kitakachoingia katika moja ya nchi zilizo katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) kitajuta.
Akizungumza  kwa sababu kikundi hicho cha uigaidi kitashambuliwa na majeshi ya nchi zote katika ukanda huo iwapo kitaanza uchokozi.
Amesema nchi za Sadc zimeamua kujizatiti katika ulinzi kwa kuunganisha majeshi yake ili kujiweka sawa na tishio lolote la ugaidi na uharamia zikiamini uchumi wake hautaimarika kama moja ya nchi itakuwa inasumbuliwa na ugaidi.
“Wakazi wa Tanga wamebahatika kuona mazoezi ya pamoja ya majeshi ya Sadc na kujionea yalivyo imara. Naamini kundi lolote la ugaidi au uharamia litakalothubutu kuingia katika nchi yoyote litajuta,” amesema.
Balozi Mahiga amesema hayo wakati akifunga mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la Ex-Matumbawe yaliyoendeshwa na majeshi kutoka nchi saba zilizo katika jumuiya ya Sadc yaliyofanyika mkoani Tanga na kuhitimishwa jana Agosti 28.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo, amesema mazoezi ya Ex-Matumbawe yenye madhumuni ya kimkakati, utendaji kivita na ki-mbinu yamefanyika nchini kwa mara ya kwanza baada ya kuendeshwa Zambia, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia, Angola na Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment