Watu walioshuhudia jengo hilo likivunjwa wamesema kazi hiyo ilianza majira ya saa 11 alfajiri.
Akizungumza katika eneo la tukio, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Rimina, Abdallah Bakari, amesema wao wanatekeleza kazi hiyo kutokana na amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.
Bakari amesema kabla ya kuvunja jengo hilo lenye maduka na ambalo pia linatumika kwa shughuli za ibada, walitoa notisi ya siku 14, ili kuwapa muda watu waliomo ndani wahamishe mali zao.
Hata hivyo, baadhi ya wapangaji wamesema hawakupatiwa taarifa jambo lililosababisha baadhi ya mali zao kuharibika wakati wa kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment