Tuesday, August 29

TAMSHA LA MICHEZO NA UTAMADUNI KUIMARISHA SEKTA YA UTALII KISIWANI PEMBA


Na Ali O. Ali
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh. Khatibu Juma Mjaja ameelezea  matumaini yake ya mafanikio katika sekta ya utalii kisiwani Pemba kupitia tamasha la michezo na utamaduni lililoandaliwa na Taasisi ya Rafiki Network.
Akizungumza mara baada ya kupokea cheti cha shukrani Ofisisni kwake Chake Chake Bwana Mjaja amesema Rafiki Network imefungua njia katika kuimarisha utalii wa ndani na nje ya nchi kutokana na kuandaa na kusimamia Tamasha la kimichezo liloandaliwa kwa ubunifu na ustadi huku likijumuisha michezo mbali mbali ya asili ambayo niburudani kwa wenyeji na kivutio kwa wageni.
Mh. Mjaja ameuomba uongozi wa Taasisi ya Rafiki Network kuhakikisha kwamba Tamasha hili linakua endelevu ambapo amebainisha kwamba kuendelea kwa tamasha hilo kila mwaka kutasaidia kukuza hali za watu katika Nyanja mbali mbali kiuchu na kiutamaduni.
Akifafanua ubunifu uliofanyika katika maandalizi ya Tamasha la kimichezo Kisiswani Pemba, Mh. Mjaja amesifu uteuzi na mpangilio wa barabara zilizotumika katika mchezo wa mbio za Baiskeli nakuongeza kwamba mpangilio huo uliwapa fursa wananchi waliowengi kuweza kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali. Afisa huyo pia amewapongeza Azam TV kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bonanza hilo.
Nae Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Pemba Maalim Suleiman Amour Suleiman amepokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Taasisi ya Rafiki Network kutokana na mchango wake mkubwa katika kufanikisha Tamasha hilo.
Taasisi ya Rafiki Network iliandaa Tamasha la kimichezo Kisiwani Pemba mnamo Julai 28-30 ambalo lilijumuisha michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na mchezo wa Ng’ombe, Mashindano ya Baiskeli, Mashindano ya  kuogelea na Resi za Ngalawa.
 Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh. Khatibu Juma Mjaja akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini kwake Chake Chake Pemba.
Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Maalim Suleiman Amour Suleiman akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini kwake Chake Chake Pemba.

No comments:

Post a Comment