Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya iliyokuwa ikimakabili Manji.
Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.
Katika kesi hiyo, upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi saba na wa mashtaka kuwa na mashahidi watatu.
Awali, Manji kupitia wakili wake Hajra Mungula aliieleza Mahakama kwamba angekuwa na mashahidi 15.
Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Ushahidi wa upande wa utetezi mahakamani unaonyesha Manji ana vyuma kwenye moyo.
Mfanyabiashara huyo katika utetezi wake alidai ana matatizo ya moyo ya kurithi kutoka kwa babu zake na alianza kuugua akiwa na miaka 26.
No comments:
Post a Comment