Friday, October 6

MFANYABIASHARA MANJI AACHIWA HURU NA MAHAKAMA BAADA YA KUKOSEKANA UTHIBITISHO ANATUMIA DAWA ZA KULEVYA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji jijini Dar es Salaam leo mara baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake yaliyokuwa Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yake.



Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa shtaka lake.



 Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa hukumu na kujulikana kuwa upande wa mashtaka hawakuweza kuthibitisha kama kweli alikuwa anatumia dawa za kulevya.

.

 Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akielekea kwenye gari kwaajili ya kuondoka huku akiwa hana kosa mara baada ya kusomewa hukumu  na kuonekana kuwa hakuwa akitumia dawa za kulevya.



 Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akipanda gari akipanda gari mara baada ya kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabiri ya kutumia dawa za kulevya ikiwa upande wa mastaka walishindwa kuthibitisha shtaka hilo.



Wakili wa Manji Bi. Hajra Mungula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya mteja wake kuonekana hana kosa la matumizi ya dawa za kulevya.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment