Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema leo Ijumaa kuwa, Maji mkazi wa Tabata Segerea, alikamatwa Jumatano saa 2:30 usiku eneo la Mwenge. Amesema bastola hiyo ilikuwa na risasi sita ndani ya magazini.
Amesema awali walipata taarifa kuwa kuna watu wanakodisha silaha kwa majambazi ili wafanye kazi za uhalifu na kulipwa fedha, hivyo uliandaliwa mtego eneo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mwenge na kumkamata mtuhumiwa akitaka kukodisha kwa Sh400,000 huku akiwa tayari kuiuza kwa Sh2.5 milioni.
“Inavyoonekana silaha aliiba kwa baba yake Issack Maji (51), ambayo naye si ya kwake. Tunataka kujua aliipata wapi hivyo tumewakamata wote,” amesema Mambosasa.
Kamanda Mambosasa amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kushirikiana na rafiki yake Patrick Kilosa katika kukodisha kwa wahalifu silaha hiyo ili kujipatia kipato.
Amesema ufuatiliaji ulifanyika na kumkamata Kilosa (22) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Columbus State Community cha Marekani, mkazi wa Tabata Segerea.
“Upelelezi unaendelea ili kujua mmiliki halali wa silaha hiyo na mahojiano zaidi yanafanyika ili kubaini silaha hiyo imekodishwa mara ngapi na imetumika na watu gani,” amesema.
No comments:
Post a Comment