Friday, September 22

Mbowe: Hakuna utaratibu wa kumsafirisha Lissu



Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa sasa hakuna utaratibu wa kumsafirisha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda Marekani au Ujerumani kutokana na ushauri wa madaktari wanaomtibu.
Akizungumza leo Ijumaa jijini hapa, Mbowe amesema madaktari wamesema hawezi kwenda popote kutokana na hali yake.
Amesema baada ya awamu ya kwanza ya matibabu aliyoyapata katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7, ya pili inafanyika Nairobi, Kenya alipo sasa.
"Awamu ya tatu itaamua aende wapi ambayo itahusu mazoezi," amesema Mbowe.

No comments:

Post a Comment