Saturday, April 28

Wizara yaunda kamati kufuatilia kampuni


Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema wizara hiyo imeunda kamati kufuatilia kampuni mbalimbali zinazoingia mikataba na wasanii nchini, ili kuona wananufaika vipi, zikiwemo zilizoingia mikataba na mchekezaji maarufu nchini, Mzee Majuto.
Akizungumza bungeni leo Aprili 27, 2018 wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19, Dk Mwakyembe amesema; “Kampuni zote zilizoingia mkataba na Majuto tutapitia mikataba yao maana wasanii wetu wengi ni maarufu lakini hawana fedha.”
“Mimi ninatoa fedha zangu mfukoni kumsaidia Majuto. Majuto kwa sasa anaumwa yuko hospitali lakini hana fedha watu wanamchangia.”ameongeza
Amesema mbali na Majuto nyingine zitakazopitiwa ni zile zilizoingia mikataba na msanii Steven Kanumba (marehemu).

No comments:

Post a Comment