Thursday, April 26

Watu 7 wakamatwa kuhusiana na maandamano ya Aprili 26 Tanzania

Rais Magufuli
Image captionRais Magufuli amewaonya watakaoshiriki katika maandamano
Takriban watu saba wamekamatwa mjini Arusha nchini Tanzania wakihojiwa kuhusiana na majukumu yao katika maandamano ya kisiasa dhidi ya serikali mnamo tarehe 26 Aprili ambayo ni siku ya muungano.
Kaimu kamanda wa polisi katika eneo la Arusha , bwana Yusuph Ilembo aliambia waandishi siku ya Jumanne kwamba kukamatwa kwa saba hao kunafuatia uchunguzi uliofanywa na polisi.
Majina yao hayakuweza kuwekwa wazi lakini kulingana na bwana Ilembo wengine wao ni wanafunzi wa chuo kikuu.
''Kama serikali hatutasita , maandamano haya ni haramu hatutakubali kuhangaishwa na watu wachache ambao wanataka kuharibu amani ya Tanzania'', alisema afisa huyo.
Kukamatwa kwao kunajiri saa chache baada ya serikali ya Uingereza kutoa agizo la tahadhari kwa raia wake wanaoelekea Tanzania ikidai kuwa uwezekano wa maandamano ya kisiasa nchini humo wakati wa siku kuu ya muungano unaweza kusababisha maafa.
Mwanaharakati wa mitandao ya kijamii anayeishi nchini Marekani kutoka Tanzania, Bii Mange Kimambi ametoa wito wa kufanyika kwa maandamano dhidi ya serikali mnamo tarehe 26 Aprili kwa kile anachodai ni ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na haki za kibinaadamu.
Serikali tayari ya Tanzania imepinga madai hayo na kusema kuwa maandamano hayo yatakuwa kinyume na sheria.
Kwa upande wake, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa mara kadhaa amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale ambao watashiriki maandamano hayo.
Magufuli
Presentational grey line
Mwezi Machi mwaka huu, Polisi mjini Dodoma waliwashikilia watu wawili kwa kosa la kuhamasisha maandamano kwa njia ya mitandao.
Polisi iliwataja watu hao kuwa dereva na mkulima, ambao waliwawashutumu kwa kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha maandamano yanayopangwa kufanyika tarehe 26 April mwaka huu
Sikiliza mahojiano kati ya Mwandishi wa BBC, Sammy Awami na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto na kwanza alianza kwa kumuuliza undani wa kukamatwa kwa vijana hao.
Polisi: Kuhamasisha maandamano kupitia mtandao ni kosa la jinai Tanzania
Presentational grey line
Tarehe iliyopangwa kufanyika kwa maandamano hayo, ndio siku ambayo Tanzania inasheherekea miaka 54 ya Muungano, kati ya Zanzibar na Tanganyika, maarufu kama Tanzania Bara.
Polisi nao wameonekana wakishika doria katika miji mikubwa huku wakifanya ukaguzi hasa kwa wenye magari. Nako mjini Moshi, ambapo ni ngome ya upinzani, vikosi vya kupambana na ghasia, maarufu FFU vikiwa na silaha vimeonekana vikifanya mazoezi katika barabara kuu za mji huo. Baadhi wanahisi hii ni njia moja wapo ya serikali ya kuwatisha wananchi.

No comments:

Post a Comment