Tuesday, April 10

Wanawake 61 Dar wadai kuzaa na viongozi wa dini, wabunge


Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kati ya wanawake 480 waliozungumza na wanasheria jana Jumatatu Aprili 9, 2018, 61 wamezalishwa na kutelekezwa na wabunge pamoja na viongozi wa dini.
Makonda ametoa kauli hiyo leo Aprili 10, 2018 wakati akitoa salamu zake kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 unaofanyika leo katika viwanja vya Zakeem Mbagala.
Amesema wanawake 47 wanadai wabunge ndio wamewatelekeza na 14 wamesema kuwa wamezalishwa na kutelekezwa na viongozi wa dini.
"Katika Mkoa wangu wa Dar es Salaam, mwaka 2017 wanawake waliojifungua walikuwa 129,347 na kati ya hao asilimia 60 walitelekezwa na watoto 274 waliokotwa maeneo mbalimbali ndiyo maana tumeona tuje na mkakati huu kuhakikisha tunapambana na wale wanaume wote wanaotelekeza watoto," amesema Makonda.

No comments:

Post a Comment