Baada ya kutengenishwa na mamake muda mfupi baada ya kuzaliwa, sokwe Manno alisafirishwa hadi nchini Iraq ambapo aliishi akivuta sigara alizokuwa akipewa na wageni huku akipigwa picha na wageni waliokuwa wakimtembelea.
Sokwe huyo mwenye umri wa miaka minne pia angevalishwa nguo kama mtoto na kupewa vinjwaji na peremende
Kisha ukakuja msaada kutoka kwa makundi kadha ya kutunza wanyama, na sasa siku za Manno kama mvutaji sigara zimwekwisha baada ya kuwasili katika kituo cha kuwatunza sokwe kilicho nchini Kenya wiki moja iliyopita.
Wakati wa safari kati ya Dohuk na Erbil nchini Iraq watu waliokuwa wakimsafirisha walikuwa umbali wa kilomita 20 kutoka mji wa Mosul ambapo kuna mapigano makali kati ya jeshi la Iraq na kundi la Islamic State.
Baada ya siku kadha za safari akiwa amefungiwa kwenye kisanduku kidogo, Manno aliwasili katima kituo cha Ol Pejeta mnamo Novemba 30 ambacho kimekuwa kikiwatuza sokwe walio kwemye hatari wa kuangamia tangu mwaka 1993.
Manno ambaye anaaminiwa kuzaliwa mjini Damascus nchini Syria hajaishi maisha ya kawaida tangu auzwe kinyume cha sheria mwaka 2030 kwa dola 15,000.
No comments:
Post a Comment