Mwanamke mmoja nchini India amenusurika kifo, madaktari wanasema,baada ya kupigania maisha yake aliposhambuliwa na chui mwenye milia aliyekuwa anataka kumla mbuzi wake.
Rupali Meshram,23, alisema alipomsikia mbuzi wake akilia ,alikimbilia nje ya nyumba yake iliyopo jimbo la Maharashtra magharibi.
Alichukua fimbo na kumpiga yule chui, ambaye naye alimshambulia. Mama yake , aliyejeruhiwa pia , alimuokoa kwa kumvuta mwanae ndani ya nyumba.
Wote walipatwa na majeraha madogo na wameruhusiwa kutoka hosptalini. Mbuzi hakunusurika.
Bi Meshram alichukua picha ya 'selfie' baada ya tukio hilo, iliyotokea wiki iliopita lakini taarifa hizo ndo zimeanza kutoka hivi karibuni.
Uso wake umefunikwa na damu.
Bi Meshram alipata majeraha kwenye kichwa, miguu na mikono, lakini ameanza kupona.
"Nilidhani binti yangu angekufa," mama yake Jijabhai aliiambia idhaa ya Kihindi ya BBC, akiongozea kuwa aliogopa sana kumuona mtoto wake akiwa anavuja damu huku akimchapa viboko chui huyo.
Siku kumi baada ya tukio hilo, picha hii iliochukuliwa na BBC imemunyesha Rupali bila makovu yoyote,baada ya shambulio.
Wanasema walimuita mlinzi wa hifadhi ya wanyama pori, lakini alifika dakika 30 baadae na kukuta chui huyo ameshaondoka.
Kijiji chao kinavamiwa na wanyama pori mara kwa mara kwa sababu kipo karibu na hifadhi ya wanyama pori.
No comments:
Post a Comment