Mbunge mmoja nchini Kenya amefufua tena mjadala wa iwapo wanaume wanafaa kuwaoa wanawake wengi.
Gathoni wa Muchomba, ambaye ni mwakilishi wa wanawake kutoka kaunti ya Kiambu, amesema wanauem wakiwaoa wanawake wengi mengi ya matatizo ya kijamii yatafikia kikomo.
Video yake akitoa wito kwa watu wa jamii ya Wakikuyu kurejelea utamaduni wa kuwaoa wake wengi imesambaa sana katika mitandao ya kijamii nchini humo.
Amedai tangu jamii hiyo ilipotupilia mbali utamaduni huo, matatizo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani.
Mwaka 2014, Rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha Sheria ya Ndoa ambayo inawaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi kisheria iwapo watasajili ndoa zao kama za kitamaduni au za Kiislamu.
Wakristo hata hivyo hawaruhusiwi kuoa wake wengi chini ya sheria hiyo.
Bi Muchomba alisema wengi wa wabunge tayari wamewaoa wake wengi na “wanajivunia” jambo hilo.
No comments:
Post a Comment