Saturday, April 7

Magufuli azindua kituo cha polisi cha utalii Arusha


Arusha. Rais John Magufuli amezindua Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia mjini Arusha kitakachosaidia kutoa huduma kwa watalii na maofisa wa kibalozi.
Kituo hicho kimejengwa na wafanyabiashara wawili kwa ajili wa sekta ya utalii ili kuziba pengo lililokuwepo la kutoa huduma zenye ubora kwa wageni.
Pia, amezindua nyumba 31 za polisi mkoani humo leo Aprili 7. Ni mfululizo wa hafla za uzinduzi unaofanywa na Rais, ambapo jana alizindua ukuta wa mgodi wa Mirerani, wenye urefu wa kilometa 24.5. Ukuta huo umejengwa, kwa Sh5 bilioni.

No comments:

Post a Comment