Saturday, April 7

Kesi ya Zuma kusikilizwa tena mwezi june

Rais wa zamani wa Afrika KusiniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa zamani wa Afrika Kusini,Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini anayeshtakiwa kwa makosa ya rushwa inayohusishwa na mpango wa silaha wa mwaka 1990.
Mara baada ya Bwana Zuma kuwasili katika mahakama kuu huko Durban hapo jana kwa kipindi cha dakika 15,kesi yake ilihairishwa mpaka tarehe 8 mwezi juni.
Bwana Zuma ambaye anakabiliana na mashtaka 16 ya ufisadi,rushwa ,udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha.
Bwana Zuma alilazimika kuachia madaraka yake mwezi februari licha ya kukataa kuhusika na kosa lolote.
Wafuasi wake walisambaa mjini wakiandamana kwa ajili yake huku wapinzani wake walilalamika kwamba mahakama inachukua muda mrefu kutoa hukumu.
Baada ya kesi hiyo kusikilizwa,Bwana Zuma aliwahutubia mkusanyiko wa watu waliomsindikiza mahakamani kutoka nyumbani kwake.
"Sijawahi kuona mtu anashtakiwa kwa uhalifu, alafu mashtaka yake yanafutwa lakini baada ya miaka kadhaa ,mashtaka hayohayo yanarejeshwa" ,Zuma alisema.
"Hizi ni njama za kisiasa"
Wafuasi wa Zuma nje ya mahakama
Image captionWafuasi wa Zuma nje ya mahakama
Baada ya hapo Bwana Zuma aliongoza nyimbo na kucheza pamoja na wafuasi wake.
Mamia ya askari pia yalikuwa yanalinda
Image captionMamia ya askari pia yalikuwa yanalinda
Mpango wa silaha ulikuwa ni upi?
Mpango wa silaha ulifanyika mwaka 1999 mwaka ambao bwana Zuma alihama kutoka mkuu wa jimbo kuwa makamu wa rais.
Anashtakiwa kwa kukubali kuchukua malipo yasiyokuwa halali 783
Mshauri wake wa mambo ya fedha ,Schabir Shaikh alikutwa na hatia kwa kujaribu kuomba rushwa kwa niaba ya bwana Zuma kutoka katika kampuni ya silaha za Ufaransa na kosa hilo lilipelekea akafungwa jela mwaka 2005.
Kesi dhidi ya bwana Zuma ilifutwa muda mfupi kabla hajawania nafasi ya uraisi mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment