Sunday, April 1

Mshukiwa wa uhalifu wa kivita nchini Mali akabidhiwa mahakama ICC

Makaburi katika msikiti wa Djingareybe huko Timbuktu, yaliharibiwa na wanamgambo wa kiislamu mwaka 2012Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMakaburi katika msikiti wa Djingareybe huko Timbuktu, yaliharibiwa na wanamgambo wa kiislamu mwaka 2012
Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai-ICC iliyoko The Hague nchini Uholanzi, inasema kuwa imemzuilia mtu mmoja ambaye alikuwa akitafutwa sana kwa tuhuma za kutekeleza uhalifu wa kivita nchini Mali. Mamlaka ya Mali ndio iliyomwasilisha mtu huyo hadi Uholanzi.
Alikuwa kiongozi mkuu wa polisi wa kiislamu huko Timbuktu, wakati ilipokuwa chini ya usimamizi wa kundi moja la kijihad, miaka mitano iliyopita.
Muendesha mashtaka wa mahakama hiyo ya ICC, anadai kuwa Al Hassan Ag Abdoul Aziz Ag Mohamed, aliwadhulumu wanawake na watotio wa wasichana, kwa kuidhinisha ndoa za lazima kwa wapiganaji wa kiislamu.
Aidha, anatuhumiwa kwa kuhusika katika kuharibu maeneo ya zamani ya kihistoria katika mji huo.
Mpiganaji wa pili wa kiislamu, Ahmad Al Faqi Al Mahdi, alihukumiwa jela na mahakama hiyo hiyo ya ICC mwaka 2016, hukumu ya miaka 9 jela kwa kuhusika kwake kuharibu maeneo hayo ya ukumbusho.

No comments:

Post a Comment