Wanamgambo wa kiislamu wamefanya shambulizi kwenye kambi ya wa jeshi la Muungano wa Afrika AU nchini Somalia.
Wanamgambo hao walilipua mabomu yaliyokuwa yametegwa ndani ya magari mawili nje ya kambi ya jeshi kwenye mji wa Bulamarer, kusini magharibi mwa Mogadishu.
Wenyeji wanasema kuwa walisikia makabiliano makubnwa ya risasi ambayo yalidumu kwa zaidi ya saa tatu.
- Al-Shabab wamtafuta aliyekuwa kamanda wao
- Kenya yaanza kuangusha mabomu ‘msitu wa al-Shabab’
- Al Shabab lawaua zaidi ya wanajeshi 60 Somalia
Msemaji wa Al Shabab alisema wapiganaji wake 14 waliuawa huku wanajeshi 59 wa AU wakiuawa.
Bado madai hayo hayajathitishwa.
Miaka ya hivi karibuni, wanamgambo wa kislamu wamepoteza udhibiti wa miji ya Somalia lakini mara kwa mara hulipua mabomu na kuswashambulia walinda amani.
No comments:
Post a Comment