Meli ya abiria ya Uingereza iliyozamishwa wakati ilishambuliwa kwa bomu na ndege za Japan wakati wa vita vya pili vya dunia, imeinuliwa kutoka baharini pwani mwa Sri Lanka baada ya miaka 75.
SS Sagain, ambayo abiria wake wengi na mizigo iliokolewa mwaka 1942, imeinuliwa na kundi la wapiga mbizi kutoka kwa jeshi la wanaji wa Sri Lanka
Ilikuwa karibu umbali wa futi 35 chini ya bahari katika bandari ya Trincomalee.
Shughuli ya kuiinua meli hiyo ilichukua miezi kadhaa na ilifanywa na kikosi cha wanamaji cha Mashariki mwa Sri Lanka.
No comments:
Post a Comment