Rais John Magufuli wa Tanzania,amezindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite, yaliyopo eneo la Mererani, kaskazini mwa nchini Tanzania.
Ukuta huo ulijengwa ili kuzuia wachimbaji madini kukwepa kulipia ushuru na kuiba madini.
Rais Magufuli amesema hatosita kuzungushia ukuta sehemu yoyote yenye rasimali ambayo inaleta utata, hata ikiwa mlima Kilimanjaro yupo radhi kuulinda kwa kujenga ukuta.
Hata hivyo, Magufuli alitambua uwepo wa mvumbuzi wa kwanza wa madini ya Tanzanite ambaye hakuwahi kutambuliwa na taifa.
Bwana Jumanne Mhero Ngoma alivumbua aina hiyo ya dini la Tanzanite mwaka 1967.
Jumannne Ngoma ametambuliwa na Rais Magufuli na amemzawadia shujaa huyo milioni 100 kwa ajili ya kumsaidia kujikimu na matibabu baada ya mzee huyo kupooza sehemu ya mwili.
Aliwahakikisha wachimbaji wadogo kwamba atawajengea 'mazingira ili kusudi wafaidi na Tanzanite zaidi'
Tanzanite ni madini ya aina gani?
Ni madini ambayo ni ya kipekee kwa Tanzania haipatikani sehemu yeyote duniani.
Mauzo ya Tanzanite duniani yanafikia dola za Marekani milioni 50
Tanzanite ni jiwe yenye miaka milioni mia 6 na iligundulika Mererani, Arsuha, kaskazini mwa Tanzania, mwaka 1967
Inasemekana kuwa na upekee hata ziadi ya alhmasi.
Ukuta huo ukoje?
- Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5
- Ukuta huo wenye urefu wa mita tatu kwenda juu
- Umegharamia karibu bilioni 6 za Kitanzania
- Ilijengwa na maafisa na wanajeshi 271 wanajeshi
Nini ilipelekea kwa ukuta huo kujengwa?
Mwaka jana, ripoti ilifikishwa na tume maalum ya kuchunguza madini nchini Tanzania.
Tume hiyo iliwasilishwa kwamba Tanzania imepoteza takriban shilingi za kitanzania trilioni 188 (dola bilioni 84 za Marekani ) katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba.
Ripoti hio ilitolewa baada ya kamati maalum kuundwa kuchunguza mchanga wa madini uliokuwa katika makontena zaidi ya 200 katika bandari ya Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment