Mbunge huyo wa Kigoma Mjini ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Aprili 6, 2018 na kubainisha kuwa mpaka sasa watu mbalimbali wameshachanga Sh43.06milioni kati ya Sh75.35milioni zinazohitajika.
Amesema chama kimebaini changamoto zinazowakabili wananchi katika kata hizo baada ya Februari 19 hadi Machi 13, 2018, yeye pamoja na viongozo wenzake kutembelea kata zinazoongozwa na madiwani wa chama hicho.
“Chama kilifanya tathmini ya mahitaji, ambayo ni mifuko 1,371 ya saruji pamoja na mabati 2,680. Tunatambua kuwa wajibu wa ujenzi huu ni wa Serikali, kwa kuwa ndiyo inayokusanya kodi,” amesema.
“Lakini sisi ACT Wazalendo, kupitia falsafa yetu ya ‘Siasa ni Maendeleo’, tumeona tunao wajibu wa kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya maradhi, ujinga na umasikini hata kama hatuongozi Serikali.”
Amesema gharama za mahitaji yote ni Sh75.35, mpaka sasa kiasi kilichopatikana ni Sh 42.06milioni, “tunakukaribisha mfuasi, mwanachama, mwananchi wa kawaida pamoja na mdau wa maendeleo, ili kushiriki.”
No comments:
Post a Comment