Watu wenye silaha wameshambulia mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, huku wakilenga ubalozi wa Ufaransa na makao makuu ya jeshi la taifa hilo.
Serikali ya Burkina Faso, inasema kwamba washambuliaji wanne, wameuwawa ndani ya majengo ya ubalozi huo na watatu katika makao makuu ya jeshi.
Walioshuhudia walisema kuwa waliwaona watu wenye silaha wakitoka ndani ya gari na kuanza kumimina risasi, kabla ya kuelekea iliko ubalozi wa Ufaransa.
Taarifa kutoka kwa mwanadiplomasia mmoja, ambaye amenukuliwa na shirika moja la habari la Ufaransa - Presse, amesema kuwa hali hiyo ilidhibitiwa.
Duru kutoka kwa utawala wa Burkinabe zinasema kwamba, hakuna taarifa zozote kuhusiana na raia waliuwawa au kujeruhiwa.
Picha za kufuka kwa moshi mkubwa angani zinaonekana, huku ikiwa haijafahamika ni nani au kundi lipi lililohusika na ghasia hizo.
Idara ya usalama wa nchi hiyo chini ya maafisa wa polisi, imetoa taarifa kuwa kikosi maalum kiliitwa kukabiliana na watu hao hatari.
Meya wa mji mkuu wa Ouagadougou , Armand Béouindé, ameliambia gazeti la Ufaransa Le Monde kuwa, "washambuliaji hao walimimina risasi hadi katika makao haya makuu ya jumba la town hall na vioo vya madirisha ya ofisi yangu vikasambaratika. "bila shaka ni shambulio la kijihad," alisema, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Mmoja wa mashuhuda, Omar Zombre, ameiambia runinga moja nchini humo kuwa: "tuliwaona watu wanne ambao walijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya ubalozi huu kutokea eneo la Mashariki. Walikuwa na mavazi ya kiraia, na aina fulani ya vazi maalum na mzigo mgongoni, huku wakibeba bunduki za Kalashnikov (AK-47), zilizoonekana bayana.
"Walijaribu lakini hawakufaulu, kisha wakaelekea upande wa Magharibi wa jumba hilo. Tuliwaona wakiliteketeza moto gari. Tulipokwenda juu {katika paa la jumba} tulisikia milio ya risasi kutoka kwa gari la rashasha, [ilikuwa] hali ya kutisha."
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye alikuwa akiarifiwa kuhusiana na shambulio hilo kila dakika, amesema kuwa Ikulu ya Elysée Jijini Paris. Aliwataka raia wa Ufaransa nchini humo kufuata ushauri unaotolewa na ubalozi mjini Ouagadougou na kuwa mbali na eneo la shambulio hilo.
Wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini humo pia wametumwa huko.
Waziri wa Mashauri ya nchi za kigeni wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, ameiambia ameiambia runinga ya ICI kwamba hakuna "raia yeyote wa Ufaransa aliyejeruhiwa au kuuwawa".
Kambi hiyo ya jeshi na majengo ya ubalozi wa Ufaransa- ambayo pia iko karibu na Ofisi ya Waziri mkuu- yako katika eneo la kilomita moja kutoka nyingine.
Runinga ya taifa hilo inasema kuwa, Waziri mkuu yuko salama.
Ubalozi wa Marekani mjini humo, umewashauria raia kutahadhari na kujificha.
Katika miaka miwili ya nyuma, mji wa Ouagadougou umeshambuliwa na wapiganaji wa kiislamu.
Taifa hilo lililoko Afrika Magharibi, pia lilikabiliwa na jaribio la mapinduzi, lililotibuka mwaka 2015. Mapema wiki hii, kesi ya waliopanga jaribio hilo la mapinduzi ilianza, lakini ikaahirishwa baada ya mawakili wao walipoondoka nje ya mahakama hiyo, wakilalamika kupinga mahakama ya kijeshi.
No comments:
Post a Comment