Friday, March 2

Vodafone na Nokia kuweka mtandao wa 4G kwenye Mwezi

Moon landerHaki miliki ya pichaVODAFONE
Image captionMtambo wa kutua kwenye Mwezi (kushoto) na mtambo wa kupeleleza (chini kulia)
Kampuni maarufu za simu za mkononi Vodafone na Nokia zimetangaza mpango wa kuweka huduma ya mtandao wa 4G kwenye mwezi.
Mpango huo unatarajiwa kukamilishwa mwaka 2019.
Mtandao huo utatumiwa na mitambo ya kupeleleza anga za juu kutuma picha, video na maelezo hadi duniani.
"Tunatuma mitambo hii miwili kwenye Mwezi na tutakusanya data, video za HD na picha nyingi zenye maelezo na umuhumu kisayansi. Tatizo ni kwamba hatuwezi kuzituma moja kwa moja kutoka kwa mitambo hiyo hadi duniani. Hii ni kwa sababu itatumia nishati nyingi," amesema Kate Arkles Gray wa shirika la PTScientists.
"Kwa hivyo, kutumia mtandao wa 4G kwenye Mwezi kutatuwezesha kutuma data, video na picha hizo hadi kwenye mtambo wa kutua kwenye Mwezi ambao una nishati nyingi, na unaweza basi kuvituma hadi duniani."
"Kwa kufanya hivyo, tutaweza hata kuzitazama video hizo za HD moja kwa moja kutoka kwenye Mwezi tukiwa hapa duniani.
MweziniHaki miliki ya pichaHISANI
Wengi wameshangaa ni kwa nini kampuni hizo zimeangazia mradi huo badala ya kuangazia zaidi kufikisha huduma ya simu katika maeneo mengi duniani ambayo bado hayana huduma hiyo.
"Naam, ni kweli naegemea upande mmoja kwa sababu mimi hufanyia kazi kampuni inayoangazia upelelezi wa anga za juu lakini kuna mambo na vitu vingi sana ambavyo tunavitumia kwa sasa duniani kila siku ambavyo vilianza kama teknolojia ya kutumiwa anga za juu," anasema Bi Gray.
MweziniHaki miliki ya pichaHISANI
Anatoa mfano wa teknolojia inayotumiwa kwenye kamera za sasa kwenye simu ambazo hutumia sensa ambayo iliundwa kwa ajili ya kutumiwa anga za juu.
"Huwezi kujua ni mambo gani ya kushangaza ambayo tunaweza kujifunza kwa kufanya sayfari, kama hii yetu, ya kwenza kupeleleza kwenye Mwezi."
Teknolojia ya 4G ni nini?
Teknolojia hii ya kasi ilianza kutumiwa 2010 na iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu.
G kwenye tarakimu hii inawakilisha 'Generation', yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.
Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.
Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.
Afrika Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.
5G ndiyo mwendo kasi?
Hii ndiyo teknolojia ya kasi zaidi ya mtandao wa simu kwa sasa.
Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.

No comments:

Post a Comment