Friday, March 2

Kijana aliyegeuza taka za plastiki kuwa malighafi Tanzania

Edgar Edmund Tarimo,17, ni mshindi wa Anzisha Prize 2017
Image captionEdgar Edmund Tarimo,17, ni mshindi wa Anzisha Prize 2017
Akiwa na umri mdogo tu chini ya miaka 17, Edgar Edmund Tarimo ameweza kubuni na kutengeneza mashine ya kutengenezea vigae vya sakafu, (Paving Blocks), kwa kutumia taka za plastiki na mchanga.
Kupitia ubunifu wake huo, ameweza kupunguza kiasi kikubwa cha taka za plastiki mitaani na kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira zinazotokana na taka hizo.
Na Kupitia kampuni yake ya Green Venture tayari ameajiri wafanyakazi sita na kuweza kutoa kipato kwa takriban watu themanini, ambao hufanya kazi ya kumkusanyia taka za plastiki.
Edgar anasema alianza ujasiriamali akiwa na mtaji wa shilingi za Kitanzania elfu 40, na tayari ameweza kushika mpaka kiasi cha milioni nne za Kitanzania.
Vigae (paving Blocks) vilivyotengenzwa na plastiki
Image captionVigae (paving Blocks) vilivyotengenzwa na plastiki
Edgar Edmund ambaye amehitimu kidato cha nne mkoani Arusha mwaka uliopita, alikanza kutengeneza mashine hiyo aliyoivumbua miaka mitatu iliyopita, kutokana tatizo la mafuriko lililowahi kutokea na baadhi ya watu nyumba zao zilisombwa na maji, kutokana na kuokuwa imara na pia uchafu wa plastiki ulikuwa ukiathiri mazingira, kutokana na kusombwa na kutawanywa na maji kutoka maeneo mbalimbali wakati wa mafuriko hayo.
''Nilifikiria jinsi ya kutatua matatizo mawili kwa suluhisho moja ndio nikafikiria jinsi gani naweza kutumia taka kutengeneza bidhaa za ujenzi ambazo zinaweza kuwa za bei rahisi ili watu watumie kujengea katika nyumba zao ziwe imara, na pia kupunguza uchafu wa mazingira kwa kukusanya taka hizo za plastiki na kuzitumia.''
Mashine anayotumia kuyeyusha plastiki
Image captionMashine anayotumia kuyeyusha plastiki
Kabla ya kutengeneza mashine hiyo, alikuwa akitumia jiko la kawaida la mkaa na sufuria kuweza kuyeyusha plastiki hizo.
Kwa upande wa mama yake, Emiliana Tarimo anasema hakutegemea mwanae kufikia mafanikio hayo, kutokana na jinsi alivyoanza na changamoto alizokutana nazo.
Hata hivyo anasema kutokana na umri wake mdogo, anamshauri aendelee na masomo yake na kuhitimu vizuri, ili aweze kupata mafanikio zaidi ya kazi yake.
Ameiomba serikali kuweza kusaidia mtoto huyu, kutopoteza kipaji chake na kuweza kuilinda kazi yake hiyo, kutokana na umri wake mdogo, wa chini ya miaka 18.
Mwaka jana wa 2017, Edgar Edmund alifanikiwa kupata tuzo ya Anzisha Prize baada ya wazo lake la kibiashara la kubadilisha taka za plastiki, kuwa malighafi ya kutengenezea vigae (paving Blocks) kwa kuchanganya na mchanga, kushinda.

No comments:

Post a Comment