Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ikulu leo Machi 7,2018 Rais pia ametuma rambirambi kwa wana CCM, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo.
Rais Magufuli katika salamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga ameiombea familia ya marehemu na wote walioguswa na msiba huo kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi cha majonzi.
Dk Kabourou aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Kigoma amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Machi 7,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Amesema Dk Kabourou atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, alipokuwa mbunge wa Kigoma Mjini na wa Bunge la Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment