Monday, March 12

Jeshi la Myanmar latuhumiwa kutwaa maeneo ya Warohingya jimbo la Rakhine

Wanajeshi wa MyanmarHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wa Myanmar
Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limedai kuwa jeshi la Myanmar limejenga kituo katika vijiji ambavyo watu wa Rohingya wamelazimishwa kuyakimbia makaazi yao.
Wanaharakati wa shirika hilo wamesema watu walioshuhudia na uchambuzi uliofanywa kupitia picha za Satellite umeonesha kuwa mwezi Januari wanajeshi wa Burma walikuwa wakisawazisha ardhi ya vijiji vya wa Rohingya kwa kuponda nyumba na hivi karibuni wamechoma moto eneo hilo.
Msemaji wa Amnesty International Tirana Hassan ameelezea hatua zillizochukuliwa katika jimbo la Rakhine kama ''Jeshi kujinyakulia ardhi''.
Serikali ya Myanmar bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na ripoti hiyo ya Amnesty International.

No comments:

Post a Comment