Afisa wa polisi nchini Marekani amempiga risasi na kumuua mtu ambaye hakuwa na silaha aliyekuwa akitembea barabarani huku suruali yake ikiwa miguuni.
Familia yake inasema mauaji hayo yanaonekana yaliyokuwa ''yamepangwa''
Kamera za video ya polisi inaonyesha kuwa Danny Ray Thomas, mwenye umri wa miaka 34, akitembea mkabala na afisa wa polisi kwenye barabara mjini Houston, Texas, Alhamisi iliyopita kabla ya kumpiga risasi.
Afisa huyo wa polisi Cameron Brewer alirudia mara kadhaa akipaza sauti "lala chini ardhini" kabla ya kufyatua risasi.
Polisi na mwathiriwa wote ni Wamarekani weusi.
Familia na Thomas inasema kuwa alikuwa na tatizo la msongo wa mawazo tangu alipofiwa na mtoto wake.
Dada yake, Kita Thomas-Smith, alihudhuria mkutano wa baraza la jiji la Houston Jumanne ambako aliwataka wanasiasa kuchukua hatua juu ya "ukatili wa polisi".
Meya Sylvester Turner alimwambia kuwa: "kusema ukweli ninahisi maumivu yako. Tunaomba msamaha kwa maisha yoyote yaliyopotezwa."
Nje ya ukumbi wa jiji, Bi Thomas-Smith alikieleza kitengo cha kamera za video za barabarani cha Houston kwamba . "anahisi kama mauaji hayo yalipangwa.
" Ni wazi hakuwa anakimbia, kuwa alikuwa anatembea, kuelekea alikokuwa afisa wala hakuwa akijaribu kumuumiza ."
Afisa huyo wa polisi Brewer, ambaye alikuwa na silaha, alipewa likizo huku polisi wakiendelea kufanya uchunguzi wa shambulio hilo la risasi.
Katika taarifa yake wiki iliyopita, Idara ya polisi ya Houston ilisema kuwa Bw. Thomas alipatikana "anatembea kwenye makutano ya barabara "yenye shughuli nyingi katika jiji''.
Polisi Brewer aliona kuwa "suruali yake ilikuwa miguuni usawa wa vifundo vya miguu, akimjongea mwenyewe huku akigonga gonga magari yaliyokuwa yakipita barabarani".
"Halafu Thomas aligonga gari jeupe kwa nguvu, na dereva wake akatoka ndani yake na kuanza kupigana na mshukiwa," alielezea taarifa ya polisi ya Houston.
Ndipo afisa wa polisi alipoona tukio hilo na kusimamisha gari lake kuingilia kati.
"Kwa kuhofia usalama wake, afisa alichukua silaha yake ya kazi na kumpiga risasi moja Thomas kwenye kifua chake ," alisema afisa wa polisi wa Houston, anayeongoza uchunguzi wa tukio hilo.
Katika video tofauti iliyochukuliwa na mtu aliyekuwa amesemama kando na kuchapishwa katika jarida la matukio ya barabarani juma lililopita, watazamaji wa tukio hilo waliokuwa kwenye kituo cha basi wanasikika wakicheka huku wakibashiri kuwa afisa wa polisi atatumia bunduki dhidi yake.
" Anakaribia kupigwa risasi ya kumtuliza," anasema Kaaryn msichana alipokuwa akichukua video ya tukio
"Milio ya risasi inasikika".
Anasikika akiuliza kama mtu ambaye haamini kilichotokea: "amempiga risasi mwanamume?
"Lazima amepigwa risasi ya kumtuliza!
"Hakupaswa kumpiga risasi mtu mtaani."
Kulingana na ndugu zake , mkewe Bwn. Thomas aliwauwa watoto wake wawili mwaka 2016.
Anasubiri kesi ya mauaji, ambayo yalitokea wakati Bw Thomas alipokuwa jela akitumikia kifungo cha miaka mitatu kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment