Dk Mpango ametoa ombi hilo leo Machi 2 wakati alipokutana na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Felipe Jaramilo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango aliishukuru WB kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk John Pombe Magufuli katika kutekeleza miradi ya maedeleo nchini.
Dk Mpango ameeleza kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa kiwango cha kati ya asilimia sita hadi saba kwa mwaka na hivyo kuiwezesha Serikali kuendelea na utoaji wa huduma za jamii na kuwekeza katika miradi ya maendeleo.
“Pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi, Taifa bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango cha umaskini bado kiko juu, ukuaji mdogo wa sekta ya kilimo na kupungua kwa mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi,”amesema.
Wakati huohuo, Dk Jaramilo aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri inayofanya ya kusimamia uchumi mpana na kuongeza makusanyo ya ndani ambayo yanasaidia upatikana fedha kwa ajili ya kugharamia uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aliishauri Serikali kuwekeza zaidi katika rasilimali watu na miundombinu ili Taifa liweze kuhimili ushindani wa kimataifa wa dunia na kujenga uchumi unaokua na endelevu.
No comments:
Post a Comment