Akizungumza wakati wa kongamano la kitaaluma lililowakutanisha wataalamu wa upasuaji kutoka Hospitali ya Apollo na Mloganzila leo Machi 12,2018 mganga mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Kambi amesema Mamc ina vifaa tiba vya kutosha kuweza kuhudumia Watanzania.
"Tunahitaji kupunguza msongamano katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete –JKCI na kutoa tiba kwa Watanzania wengi zaidi wanaohitaji huduma hizi, hivyo nawashauri Apollo mfikirie namna ya kuanzisha kambi kubwa za upasuaji hapa Mamc, vifaa tunavyo na madaktari wapo wa kutosha," amesema Profesa Kambi.
Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Apollo, Dk Vijay Diktish amesema wameupokea ushauri huo na kwamba wanafikiria kuanzisha kambi hizo mapema mwaka huu.
Amesema wakati wakitoa mafunzo kwa madaktari 11 kutoka Tanzania walifikiria namna ya kuwajengea uwezo zaidi kwa vitendo, hivyo lazima wawaunge mkono mafunzo kwa vitendo watakaporejea nchini
No comments:
Post a Comment