Wednesday, December 6

Wapalestina: Rais wa Marekani Donald Trump akiitambua Jerusalem amani itavurugika Mashariki ya Kati

The Israeli flag flutters in front of the Dome of the Rock mosque and the city of Jerusalem, on December 1, 2017.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionIsrael imeuchukulia Jerusalem kuwa mji mkuu wake, lakini Wapalestina wanataka Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wake watakapofanikiwa kuunda taifa lao.
Viongozi wa Wapalestina wametaja hatua inayosubiriwa ya Rais wa Marekani Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel kuwa hatari kwa juhudi za kutafuta amani Mashariki ya Kati.
Lakini waziri mmoja wa Israel amefurahia hatua hiyo na kusema mataifa mengine yanafaa kuufuata mfano wa Marekani.
Bw Trump anatarajiwa kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel kwenye hotuba baadaye leo.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema hali ambayo imeendelea kuwepo kuhusu Jerusalem inafaa kuheshimuwa, kaumbatana na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Israel imekuwa kwa muda mrefu ikiuchukulia mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wake, lakini Wapalestina wanataka Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wake watakapofanikiwa kuunda taifa lao.
Jerusalem Mashariki ilitekwa kutoka kwa Jordan baada ya vita vya 1967.
Kwa kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, Marekani itakuwa inaenda kinyume na sera yake ya muda mrefu kwamba hatima ya mji huo mtakatifu inafaa kuamuliwa kama sehemu ya mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.
Hatua hiyo - ambayo iliahidiwa na Trump wakati wa kampeni - inatishia kuzua hisia kali miongoni mwa washirika wa Marekani katika ulimwengu wa Kiislamu na kusababisha maandamano na pengine hata machafuko.
US President Donald Trump, visiting Jerusalem in May 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionTrump aliutembelea mji wa Jerusalem Mei 2017
Mwakilishi wa Wapalestina Uingereza Manuel Hassassian ameambia BBC kwamba mabadiliko hayo ya sera ya Marekani kuhusu Jerusalem ni kama "busu ya kifo" kwa suluhu ya kuwepo kwa mataifa mawili (taifa la Wayahudi na Wapalestina) ambayo imekuwa ikijadiliwa katika mchakato wa kutafuta amani Mashariki ya Kati.
Amesema hatua hiyo ni kama "kutangaza vita".
"Huu ndio msumari wa mwisho kwenye jeneza. Sisemi kutakuwa na vita kwa maana ya vita vya kawaida, lakini ninamaanisha vita vya kidiplomasia."
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu bado hajazungumzia hatua ya Trump hadharani lakini waziri wa elimu wa Israel Naftali Bennett amesema ni "hatua kubwa katika kufikia amani kwenye kanda" na akazihimiza nchi nyingine zihamishe afisi zao za kibalozi.
Ameongeza kuwa hilo litawalazimisha "maadui" wa Israel kukubali kwamba mji wa Jerusalem haufai kugawanywa.
Lakini Papa Francis amesema mashauriano yatafanikiwa kupitia tu "kutambua haki za watu wote" katika kanda hiyo.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahidi kuzungumzia hatua hiyo ya Trump baadaye.
Jews and Arabs on the Temple Mount/Haram al-SharifHaki miliki ya pichaRRODRICKBEILER
Image captionHakuna taifa lililowahi kutambua Israel kama mmiliki halisi wa Jerusalem yote
Msimamo wa Uingereza kuhusu Jerusalem hata hivyo haujabadilika, waziri mkuu huyo aliambia Bunge - kwamba hatima ya mji huo inafaa kuamuliwa kwenye mazungumzo na kwamba inafaa kugawanywa mara mbili na kuwa mji mkuu wa Israel na mji mkuu wa taifa la Wapalestina.
Kwa nini Jerusalem inazozaniwa?
Mzozo kuhusu Jerusalem ni moja ya mzozo mkubwa kati ya Israel na Wapalestina ambao wanaungwa mkono na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.
Mji huo una maeneo matakatifu ya dini tatu zenye kufuata imani ya Ibrahim - Uyahudi, Ukristo na Uislamu - sana maeneo mengi yanapatikana Jerusalem Mashariki.
Jerusalem
Israel ilitwaa eneo hilo kutoka Jordan wakati wa vita kati ya nchi za Kiarabu na Israel mwaka 1967 na imekuwa ikiuchukuliwa mji wote kuwa mji wake mkuu ambao hauwezi kugawanywa.
Kwa mujibu wa maafikiano wakati wa mazungumzo ya amani ya Wapalestina na Waisraeli ya 1993, hatima ya mji huo ilifaa kuamuliwa wakati wa hatua za mwisho za mazungumzo.
Hatua ya Israel kudhibiti Jerusalem yote haijawahi kutambuliwa kimataifa na nchi zote zina afisi za kibalozi Tel Aviv.
Tangu 1967, Israel imejenga makazi kadha ya Wayahudi na kuna takriban walowezi 200,000 wa Kiyahudi eneo hilo. Makazi haya yamekuwa yakishutumiwa na jamii ya kimataifa.
Hatua ya Marekani kuitambua Israel itaonekana kutilia mkazo msimamo wa Israel kwamba makazi hayo ni halali.
Marekani inapendekeza nini?
Maafisa wa utawala wa Trump wamesema kwa kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, serikali ya Marekani itakuwa inakiri tu "uhalisia wa kihistoria na wa sasa".
Hata hivyo, mipaka halisi katika mji huo badi itaamuliwa kwenye maafikiano ya mwisho ya amani, maafisa hao wanasema.
Aidha, hadhi na hatima ya maeneo matakatifu ya kidini haitaathiriwa.
Wengine wamesema nini?
Palestinian protesters burn pictures of US President Donald Trump at the manger square in Bethlehem on December 5, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPalestinian protesters burned pictures of Donald Trump on Tuesday
  • Saudi Arabia, mshirika wa Marekani, imetaja hatua hiyo kama "uchokozi wazi kwa Waislamu"
  • Kiongozi wa Hamas Ismail Haniya amesema hatua hiyo itavuka "mipaka yote"
  • China imeonya dhidi ya kuongezeka kwa uhasama Mashariki ya Kati
  • Mfalme Abdullah wa Jordan amesema hatua hiyo "itahujumu juhudi za kufufua mazungumzo ya amani"
  • Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi amemsihi Trump "kutofanya vigumu hali kanda hiyo"
  • Uturuki imeomba kuwe na mkutano mkuu wa nchi za Kiislamu Desemba kujadili hatua hiyo
  • Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema "Waislamu wanafaa kuungana pamoja dhidi ya njama hii kuu"

No comments:

Post a Comment