Wednesday, December 6

Ndege ya Marekani ya B-1B ya kuangusha mabomu yawaonyesha ubabe Korea Kaskazini

A US Air Force B-1B Lancer assigned to the 37th Expeditionary Bomb Squadron, takes off to fly a bilateral mission with Japanese and South Korea Air Force jets in the vicinity of the Sea of Japan, from Andersen Air Force Base, Guam, 10 October 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNdege ya Marekani ya B-1B yaonyesha ubabe Korea Kaskazini
Jeshi la Marekani limerusha ndege yake ya kuangusha mabomu aina ya B-1B katika anga ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani.
Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu kuonyesha ubabe baada ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini au majaribio ya mabomu ya nyuklia.
In this handout image taken on 3 December by U.S. Air Force and released on 4 December, U.S. Air Force F-16 Fighting Falcon (R) and F-35A Lightning II fighter jets taxiing at Kunsan Air Base on 3 December 2017 in Kunsan, South Korea.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege za vita za F-16s na F-35As pia zimeshiriki mazoezi
Zaidi ya ndege 200 na maelfu ya wanajeshi wanashirikia katika mazoezi hayo ya kijeshi ambayo yatakamilika siku ya Ijumaa.
Pyongyang ambayo mara nyini hukashifu mazoezi ya pamoja ya Marekania na Korea Kusini, imeyataja mazoezi ya sasa kuwa uchokozi wa vita vya nyuklia.
Misukosuko imekuwa ikiongezeka tangu lifanyike jaribio la kombora mwezi uliopita lililosababisha lawama za kimataifa na onyo kutoka Marekani kuwa Korea Kaskazini itaharibiwa aabisa ikiwa vita vitatokea.

No comments:

Post a Comment