Wednesday, December 6

Mlanguzi mkuu wa mihadarati Rogerio 157 akamatwa Brazil

Ilani ya kukamatwa kwa Rogerio 157
Image captionIlani ya kukamatwa kwa Rogerio 157
Maafisa wa usalama nchini Brazil, wamemtia mbaroni mmojawepo wa walanguzi wakuu wa dawa za kulevya katika mji mkuu Rio de Janeiro.
Idara ya usalama iliwatuma zaidi ya maafisa 300 wa polisi kumkamata mlanguzi huyo.
Picha na video kwenye runinga nchini Brazil zinaonyesha Bwana Rogerio Avelino da Silva, maarufu kwa jina Rogerio 157, akiwa amefungwa pingu.
Amekuwa akisakwa kwa miezi kadhaa kwa madai ya kuhusika na ulanguzi wa mihadarati, kupata pesa kwa njia ya haramu, unyang'anyi na mauaji.
Majaribio ya awali ya kumnasa yalikuwa yakitibuka.
Binti Rocinha favela au shanty town, alikamatwa mwezi SeptembaHaki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionRocinha Favela au Shanty Town, alikamatwa mwezi Septemba
Mwezi Septemba, mtu mmoja aliyekuwa na bunduki mwaaminifu kwa Rogerio 157, alikabiliana vikali katika kisa cha ufyatulianaji wa risasi barabarani na makundi hasimu ya magenge ya mihadarati.
Kisa hicho kilitokea baada ya kufungwa kwa kinara mmoja mkuu aliyekuwa akiliongoza genge moja kuu la ulanguzi wa dawa za kulevya maarufu kama Rocinha Favela au Shanty Town.

No comments:

Post a Comment