Maafisa wa serikali ya Marekani wamesema kuwa rais Donald Trump, leo atautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Ikulu ya White House imethibitisha kuwa rais Donald Trump pia atazungumza kuhusu juu ya kutangaza rasmi kuhamishia kwa ubalozi wa Marekani Jerusalem.
Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya white house sarah sanders amesema kuwa Trump alizungumza na baadhi ya viongozi siku ya jumanne kuhusu mpango yake ya kuhamishia ubalozi huo kutoka Tel Aviv kuupeleka Jerusalem.
- Kwa nini mji wa Jerusalem ni mtakatifu?
- Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel
''Amezungumza na baadhi ya viongozi asubuhi ya jana na atendelea kuwa na majadiliano na wadau wanaohusika lakini atafanya maamuzi yenye umuhimu kwa Marekani''
Wakati huo huo viongozi wa Palestina, Misri, Jordan na Saudi Arabia, wametoa onyo kwa rais Trump kuwa kuhamishia ubalozi huo Jerusalem kutadhoofisha kabisa juhudi za kuleta amani mashariki ya kati.
Trump aliwapigia simu viongozi hao na kuwaambia juu ya matarajio yake hayo ya kuhamisha ubalozi.
Kiongozi mkubwa wa Hamas khalili al haya, amewataka wote wanounga mkono palestina kuungana na kupinga jitihada zozote za kuhamishia kwa ubalozi huo mjini Jerusalem
'' suala la Jerusalem ni suala la msingi sana , leo hamas inawataka watu wote wanaounga mkono palestina na kusimama pamoja juu ya suala hili, kuna jitihada zinazofanywa na hamas nje ya palestina ,Lebanon na sehemu nyingine za walipo wahamiaji.
Tunawataka wote kupinga mpango huu wa marekani kuhusu Jerusalem''
Mbali na kuwa jerusalem imekua haitambuliki kimatifa , Israel imekua ikitambua jerusalem kama mji wake mkuu
Nao palestina wamekua wakidai jerusalem mashariki kuwa ni mji mkuu wao wa baade.
Marekani itakua nchi ya kwanza kutambua jerusamelem kama mji mkuu tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka 1948
No comments:
Post a Comment