Saturday, December 2

Pole Carzola sasa ni bora urudi Llanera


Hivi unadhani Santiago Carzola anajisikiaje pale mtoto wake India Ursula akimuuliza baba mbona huendi kazini? Katikati mwa msimu jibu rahisi la Carzola kwa mwanae lilikuwa "mwanangu nitarudi kazini mwezi wa kumi"
Mwaka mzima umepita na Carzola bado hajarudi kazini. Swali gumu zaidi kwa mwanae ni "baba mbona kwenye picha ya pamoja ya Arsenal ya msimu hu haupo? Carzola itabidi amwambie nitarudi kazini mwakani?
Mwaka 1993 dunia ilipata pigo baada ya moja wa washambuliaji hatari kwa wakati huo Marco Van Basten alipomua na kukaa nje kwa miaka miwili kabla ya kutangaza kustaafu soka akiwa na miaka 28 tu.
Van Basten alitikisa dunia akiwa na Ajax na baadaye AC Milan akkiwa amefunga mabao 300, lakini majeruhi yalimlazimisha kuacha soka 1995.
Michael Owen aliteseka na majeruhi maisha yake yote ya soka. Alipofika mwaka 2013 aliona bora awe Dk Leakey wa England ili acheze mpira wa mdomoni kwenye vituo vya Tv baada ya mateso ya misuli kwa kipindi kirefu.
Mwaka 2007 Dr Richard Steadman alimweleza Ji Sung Park kuwa opereshen yake ya goti itamweka benchi mwaka mmoja, haikuwa taarifa nzuri.
Huyu Dk maarufu aliwahi kuwatibu akina Ronaldo, Ruud van Nistelrooy, Michael Owen na Alan Shearer na kuwaeleza wazi kuwa matatizo yao ya misuli yatahitimisha soka lao.
Carzola naye tangu Oktoba mwaka jana hayupo uwanjani. Dr wake ndugu Roman Cugat huenda ndiye mwenye majibu sahihi kwa mtoto wa Carzola ambaye anamuuliza baba kwanini huendi kazini.
Jibu la Cugat kwa mtoto wa Carzola ni moja tu. Amweke wazi kama Steadman alivyofanya kwa akina Delima. Amweleze ukweli kuwa baba hawezi kurudi uwanjani mapema hivyo atarudi Lugo de Llanera in Oviedo (nyumbani kwao).
Michael Owen aliumia mnamo Aprili 12, 2002 akiwa na Liverpool kule Leeds. Mwaka 2007 alikaa nje ya uwanja takriban siku 315. Achana na 2012 ambapo alikaa nje kwa siku 129.
Maisha haya ya Owen kushindwa kuishi kwa amani ndiyo yanamrudisha Carzola Llanera. Wakazi wa Asturias walizoea kumuona Carzola akikatiza misitu ya akina Vidic, Terry na Cahil. Wamemisi kumuona Carzola akimpa Furaha Wenger.
Dr wake Roman Cugat ameshauri Carzola aachane na soka. Huu ni uamuzi mgumu sana kwake. Tokea mwezi wa 10 mwaka jana ilisemekana Carzola atatumia siku 346 akiwa benchi.
Lakini kutokuwepo kwa Carzola kwenge picha ya pamoja ya Arsenal msimu huu basi huenda asiwepo mpaka mwakani. Ana umri wa miaka 32 kwa sasa, unategemea nini?  Ingawa Carzola Bado anaamini kuwa pilipili ni tamu kuliko sukari, ana Imani na misuli yake ila nadhani vyema arudi llanera
Kiasi cha pesa alichokitumia kwenye upasuaji nadhani ni vyema arudi Cimavilla na fukwe za Abba Kaya kule Gijon akapunge upepo na mke wake Ursula. Aliyoyafanya ni makubwa. Asijikute Fransesco Totti.
Carzola amewekeza sehemu nyingi mno. Mwaka 2014 aliwekeza kwenye kampuni ya ardhi na makazi yenye ofisi zake Liverpool na Man United ijulikanayo kama Capital Centric Investments LLP.
Ambapo yeye na Luis Suarez, Mikel Arteta na Jose Henrique waliwekeza zaidi ya Euro milioni 50 na wanategemea kupata faida ya sio chini ya Euro 250 milioni kwa mwaka. Nadhani huu ni wakati wa yeye kusimamia mambo yake mengine ya kibiashara pamoja.

No comments:

Post a Comment