Lionel Messi hajawahi kuwa rafiki wa Cristiano Ronaldo, na hilo ni jambo la kawaida. Wachezaji wawili wanaoshinda kila msimu kuwani tuzo binafasi.
Wachezaji wanaocheza katika timu zenye upinzani wa jadi katika La Liga, wakitoka katika mataifa tofauti. Pia mjadala wa nani ni bora kati yao hajawahi kufikia mwisho.
“Hatuna mahusiano yoyote,” Messi alisema wakati akipokea tuzo ya Kiatu cha Dhahabu ya kuwa mfungaji aliyefunga mabao mengi zaidi Ulaya.
“Urafiki unajengwa kwa kutumia muda mwingi pamoja na kujua vizuri kila moja. Tumekuwa tukionana wape kwenye sherehe za kupokea tuzo tu. Kila kitu kipo safi, lakini maisha yetu hayaingilia mara kwa mara.”
Messi yuko sahihi, lakini hiyo haiwezi kumzui kufaidika na mafanikio yanayotegenezwa na Ronaldo katika masoko yaliyochangia kwa Messi kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu utakaomalizika akiwa na miaka 34. Hiyo ni moja ya njia nyingi ambazo Ronaldo anamsaidia moja kwa moja au kwa njia nyingine kwa Messi kuingiza fedha nyingi.
Kwanza, Ronaldo uwepo wa Real Madrid umelazimisha Barcelona kuwabakiza nyota wake, ndani na nje ya uwanja kwa ajili ya masuala la masoko.
Ushindani wa miamba hiyo ya La Liga umekwenda mbali kwani umechangia hata kuongezeka kwa pato lao kwa mujibu wa orodha ya Forbes.
Kwa sasa Barcelona imeizidi Real Madrid katika misimamo yote kwa mwaka 2017, Lakini Forbes imeikadilia utaji wa Barcelona kufikia dola 3.64 bilioni na Real Madrid utajili wake ni dola 3.58 bilioni.
Kama watapoteza Messi hakuna ubishi kwamba thamani ya Barcelona itashuka kwa sababu klabu hiyo itapoteza pointi kutokana na kukosekana kwa mabao ya nyota huyo.
Kuondoka kwa nyota wa Brazil, Neymar kwenda Paris Saint-Germain mwanzoni mwa msimu huu kulichangia Messi kupewa mkataba mpya unaokadilia kufikia dola 830 milioni.
Pia, Ronaldo kuongeza mkataba kulichangia kupandisha thamani ya Messi. Mshambuliaji huyo Mreno alisaini mkataba mpya 2016 utakaodumu hadi Juni 2021, utakaomlipa Ronaldo hadi akiwa na miaka 36, mshahara wa dola 475,000 kwa wiki.
Forbes imekadilia gharama ya mishahara na bonasi za Real Madrid kwa mwaka zinafikia dola 50-60 milioni. Akijumla fedha zake za matangazo ya biashara Ronaldo anapokea dola 93 milioni kwa mwaka 2017 hali inayomfanya kuwa mwanamichezo anayelipwa zaidi kwa mwaka huu.
Messi yupo katika orodha hiyo akiwa watatu akipokea dola80 milioni, akiwa nyuma ya Ronaldo na LeBron James. Lakini kuongeza kwake mkataba hadi 2021 utamfanya kuingiza dola 59.6 milioni, kwa mujibu wa gazeti la Hispania la El Mundo, nyota huyo atapokea mshahara wa dola 667,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment