Sunday, December 3

Katibu wa Bunge asema hawajapokea barua ya Mtulia


Ofisi ya Bunge imesema  haijapokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai alipotafutwa naMCL Digital leo Jumapili Desemba 3,2017 ili kujua iwapo ofisi yake imepokea barua ya Mtulia amesema hawajapokea.  
Kagaigai amesema hakuna ofisi inayokuwa wazi usiku hivyo hawajapokea barua ya Mtulia ambaye taarifa ya kujiuzulu kwake aliitoa kwa vyombo vya habari jana Jumamosi Desemba 2,2017 saa mbili usiku.
Katika taarifa yake, Mtulia alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu kwa utashi wake bila shinikizo la mtu yeyote.
Mtulia ameeleza sababu za kujiuzulu ubunge na kuhama chama kuwa imetokana na uzoefu alioupata kwa miaka miwili ya ubunge.
 “Nimebaini kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi wapinzani tuliahidi kuyatekeleza,” alisema Mtulia.

No comments:

Post a Comment