Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema leo Jumanne Desemba 5,2017 kuwa wanafunzi 1,847 ni wa mwaka wa kwanza ambao mikopo yao ina thamani ya Sh6.84 bilioni na wengine 832 ni wanaoendelea na masomo lakini hawakuwa na mikopo katika miaka iliyopita.
Amesema wanafunzi wanaoendelea na masomo wamepata mikopo yenye thamani ya Sh2.76 bilioni na fedha zimeshatumwa vyuoni.
Badru amesema kutokana na kukamilika kwa rufani hizo, wanafunzi 33,200 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh108 bilioni kwa mwaka wa masomo 2017/18 hadi sasa.
Amesema bajeti ya jumla kwa wanafunzi wote kwa mwaka 2017/18 ni Sh427.54 bilioni. Badru amesema dirisha la rufaa lilifungwa Novemba 19,2017.
HESLB pia imeanza kuhamisha mikopo iliyokuwa imeelekezwa katika vyuo tofauti.
Badru amesema mikopo ya wanafunzi 590 wa mwaka wa kwanza yenye thamani ya Sh1.78 bilioni ambayo awali ilikuwa imepelekwa katika vyuo tofauti na walipo wanafunzi imehamishwa.
No comments:
Post a Comment