Akifungua mkutano wa wadau wa kilimo leo Jumatano Desemba 6,2017, Mwijage amesema benki hiyo ina mabilioni ya fedha lakini kasi ya kuwakopesha wakulima ni ndogo.
“Rais John Magufuli ameuliza wakati nikiwepo ni kwa nini mabilioni ya fedha hayakopeshwi kwa wakulima,” amesema Mwijage.
Amesema Serikali imekuwa ikikopa kwa riba kwa ajili ya kuwekeza katika benki hiyo lakini yenyewe inakaa na fedha.
“Benki imekuwa mtunzaji wa fedha badala ya kuwa mkopeshaji,” amesema Mwijage.
Waziri amesema benki hiyo imekuwa ikisema ina hofu kwamba wakopaji hawawezi kurejesha mikopo.
Amesema hayo baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Dk Yusuph Sinare kumwomba Mwijage kufikisha kilio cha wakulima kwa Serikali kutaka benki hiyo iongezewe uwezo wa kukopesha.
Mwijage amesema mpango wa Serikali wa ujenzi wa viwanda utasaidia wakulima kupata masoko ya mazao yao.
Amesema wakulima wanatakiwa kuungana kujenga viwanda vidogo vya kusindika mazao ili kuyaongeza thamani.
“Kiwanda cha kusindika nyanya kinagharimu Sh200 milioni, hivi wakulima tunashindwa kuungana na kuanzisha viwanda vya namna hii,” amehoji Mwijage.
Amewataka kuachana na dhana iliyojengeka kwamba, wakulima kazi yao itaishia katika kilimo tu bali wanaweza pia kujenga viwanda.
Mwijage amezitaka mamlaka za Serikali kuacha kufanya kazi kipolisi bali zielimishe wawekezaji na si kuwatisha. “Kuna mwekezaji alitishwa na watu wa mazingira kwamba asipofuata sheria ya mazingira atafungwa jela miaka saba.”
Mwenyekiti wa ACT, Dk Sinare amesema wakulima hawawezi kuwa na nguvu kama hawana benki imara. “Tunaiomba Serikali iiongezee nguvu benki ya wakulima iweze kutoa mikopo kwa wakulima.”
Kuhusu masoko ya mazao, amesema wakati umefika kwa Serikali kuhifadhi chakula cha kutosha na wakulima kuruhusiwa kutafuta masoko ya mazao popote pale duniani.
Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya ACT, Salum Shamte amewataka wakulima kutokuwa wazalishaji wa malighafi bali wabadilike na kuyaonge
No comments:
Post a Comment