Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe amepata wasaa wa kutembelea gereza la Wilaya ya Nzega, ambapo ameongea na Mkuu wa Magereza Bw. Anatory Kyuza na baadae kujionea msongamano mkubwa wa wafungwa katika gereza hilo.
Aidha, Mhe. Bashe amewalipia wafungwa wote waliokuwa wamefungwa kifungo cha makosa madogo hasa yale ya kushindwa kulipa Faini za kuanzia shilingi elfu Hamsini (50,000) mpaka shilingi Laki tatu(300,000) ili kusaidia kupunguza msongamano wa wafungwa katika gereza hilo.
Pia, Mhe. Bashe* alitembelea shamba la magereza ambapo alikubaliana pamoja na Mkuu wa Magereza kuweka nguvu kwenye kilimo cha Muhogo ambapo Serikali imetoa mbegu bora kwa ajili ya kilimo hicho wilayani Nzega.
Gereza la Nzega limejengwa mwaka 1923 na lina uwezo wa kuhifadhi wafungwa 50 tu lakini sasa linahudumia wafungwa na mahabusu takribani 200.
Kwa upande mwingine, Ili kuboresha makazi ya askari wa Jeshi la Magereza wilayani Nzega Mhe. Bashe ameamua kuchangia jumla ya mifuko ya Saruji 100 na matofali 10,000.
Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe amepata wasaa wa kutembelea gereza la Wilaya ya Nzega ambapo ameongea na Mkuu wa Magereza Bw. Anatory Kyuza na baadae kujionea msongamano mkubwa wa wafungwa katika gereza hilo.
Mhe. Bashe pia alipata wasaa wa kutembelea shamba la magereza ambapo alikubaliana pamoja na Mkuu wa Magereza kuweka nguvu kwenye kilimo cha Muhogo ambapo Serikali imetoa mbegu bora kwa ajili ya kilimo hicho wilayani Nzega.
No comments:
Post a Comment