Mkuya ambaye ni mbunge wa Welezo visiwani Zanzibar amesema Dk Mpango amekuwa na kawaida ya kutokujibu hoja ambazo zinatolewa na wabunge wa kutoka Zanzibar jambo ambalo limemsikitisha.
Akichangia leo Novemba 10 bungeni mjini Dodoma Mpango wa Maendeleo ya Taifa, Mkuya ambaye katika mchango wake alisikitishwa na jinsi Waziri Mpango anavyoitenga Zanzibar licha ya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“…Nadhani taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili sasa Mheshimiwa Mwenyekiti (Azzan Zungu) cha kusikitisha na fedheha kabisa ni kuona hakuna hata eneo moja lililopangiwa mpango angalau tu likaelekezwa katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Mkuya
“Hili niliseme wazi mheshimiwa mwenyekiti kupitia kwako, mheshimiwa Waziri wa Fedha (Dk Mpango) wakati tunajadili bajeti Juni mwaka huu baadhi ya wenzangu tunaotoka upande wa pili wa Muungano tulichangia maeneo fulani fulani,” ameongeza
Mkuya akichangia kwa sauti ya msisitizo amesema ‘’Lakini kwa masikitiko makubwa mheshimiwa mwenyekiti hakuna eneo hata moja lililoguswa likajibiwa hoja angalau kule upande wa pili wakasikia na mimi nilichukua hatua kwenda kumuuliza mheshimiwa waziri wa fedha mbona angalau hata hoja mbili ili nao waone ni sehemu ya muungano.”
“Mheshimiwa waziri aliniambia muda ni mchache na majibu yalikuwa mengi, nilijisikia vibaya kwa sababu kama una ‘responsibility’ ya pande mbili za Jamhuri maanake angalau ungechukua hata hoja mbili ukazijibu sasa aliniambia kabisa muda mchache hoja zilikuwa nyingi sasa nitakupa document…nimesikitika,” amesema
Mkuya amesema sasa tunachangia hapa na nimeonda tendency ya wabunge ambao wanatoka upande mwingine wanachangia, tuombeni Mungu angalau hoja mbili tatu zijibiwe muda uwepo.
“Kuna masuala mengine hayahitaji lazima iwe ni wizara inayoshughulika na Muungano, kuna mambo mengine ishu zingine zinahitaji coordination za pande mbili hivi kweli kama hii ya utalii kunaweza kuwa na project bila kuihusisha Zanzibar haipo?
No comments:
Post a Comment