Thursday, November 16

Watu 11 waliofariki ajali ya ndege Ngorongoro wapatikana


Ngorongoro. Miili 11 ya abiria na rubani wa Ndege ya Shirika la Coastal Aviation iliyoanguka eneo la Creta ya Empakai yapatikana.
Ndege hiyo iligonga mlima wa kingo za creta hiyo ilianguka saa saba mchana kutokana na matatizo ya hali ya hewa.
Ilikuwa inatoka Kilimanjaro kwenda Seronera  Serengeti ikiwa na abiria 11 na wote wamefariki.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo amesema zoezi la kutafuta miili limekwenda vizuri.
"Miili yote imepatikana na tutaipeleka Karatu na baadaye Arusha," amesema.
Naibu Mhifadhi wa Ngorongoro, Dk Maurus Msuha amesema wamefanikiwa kuipata miili na kuitoa eneo la ajali kutokana na ushirikiano mkubwa na wenyeji.
"Tuliwaomba kulala hapa wenyeji jana kuilinda isiliwe na wanyama na hadi leo tumeikuta miili salama," amesema.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Lunda Mollel amesema ndege hiyo kabla ya kuanguka ilikuwa inazunguka kutoka eneo la milima zaidi ya dakika 20 hadi baadaye kuanguka baada ya kugonga mlima.

No comments:

Post a Comment