Friday, November 3

Waendesha mashtaka wataka Oscar Pistorius aongezewe kifungo

Oscar PistoriusHaki miliki ya pichaREUTERS
Waendeshaji mashtaka nchini Afrika Kusini wameiomba mahakama iongeze kifungo cha mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ambaye alifungwa kwa makosa ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Wameambia Mahakama ya Juu ya Rufaa kwamba kifungo cha miaka sita ambacho alihukumiwa bingwa huyo wa Olimpiki ni "laini mno" na kwamba badala yake anafaa kufungwa miaka 15.
Mawakili wa mfungwa huyo wamesema kifungo hicho alichohukumiwa na mahakama ya chini kinamfaa.
Pistorius alidai kwamba alimpiga risasi Bi Steenkamp kimakosa akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa ameingia nyumbani kwao Siku ya Wapendanao mwaka 2013.
Mahakama ya chini ilikosa kumhukumu kifungo cha miaka 15 kilichopendekezwa ikitaja baadhi ya mambo kwa mfano kumrekebisha na pia kwamba alionesha majuto. Mahakama ilisema hayo yalizidi lawama kutokana na hali kwamba hakufyatua risasi ya onyo.
Lakini mwendesha mashtaka Andrea Johnson amesema kifungo hicho hakijalingana na uzito wa kosa alilolitenda.
Pistorius, 30, hakuwa kortini Bloemfontein.
Reeva Steenkamp - 7 February 2013Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSteenkamp alikuwa mwanamitindo
Anaendelea kuzuiliwa katika gereza moja Pretoria.
Awali, alikuwa amefungwa miaka mitano kwa mauaji bila kusudia mwaka 2014 lakini akapatikana na makosa ya mauaji baada ya rufaa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment