Wakili mmoja wa kike nchini Zimbabwe ameanzisha kesi ya kufutilia mbali lobola au mahari akisema kuwa ni mila iliopitwa na wakati ambayo inawafanya wanawake kuonekana kama mali kulingana na gazeti la serikali la Herald.
Priccilar Vengesai anaamini kwamba iwapo utamaduni huo utaendelea ,familia zote za mume na mke zinafaa kulipa mahari kwa maslahi ya usawa wa kijinsia, gazeti hilo limeongezea.
Amewasilisha malalamishi yake katika mahakama juu, mahakama ya kikatiba akitaka kusikilizwa kwa kesi yake kwamba utamaduni huo unakiuka haki za raia.
Gazeti hilo limemnukuu bi vengesai akisema kwamba anataka kuolewa na hataki kupitia aliyopitia alipokuwa katika ndoa.
Sikushiriki katika kuuliza gharama ya mahari. Sikupewa fursa ya kuuliza kwa nini mharai ilitolewa.
Hali yote hiyo ilinifanya mimi kuonekana kama ''mali'' ambapo kiwango cha thamani yangu kilipendekezwa na wajomba zangu na mume wangu akalipa.
Hatua hii ilinivunja moyo na hali hiyo kuniweka chini ya udhibiti wa mume wangu kwa kuwa najihisi kwamba nilinunuliwa.
Mimi natoka katika kabila la Shona na ningependelea kuingia katika ndoa mara tu kesi hii itapokamilika na uamuzi kutolewa.
Chini ya utamaduni wa kabila la shona, Lobola ama mahari lazima alipiwe mwanamke kabla ya ndoa kukubalika katika familia na jamii.
Katika hali ambapo Lobola haijalipwa, wazazi na jamaa wa familia ya mwanamke hawataruhusu ndoa hiyo kuhalalishwa chini ya sheria ya ndoa.
No comments:
Post a Comment