Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkurugenzi wa taasisi ya AL Hikma Nurdeen Kishki amesema kuwa kwa sasa waumini wake pamoja na jamii inayozungumza wanaweza kupata mawaida yake, hadhara, hotuba na hadithi mbalimbali kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Shekh Kishk ameweka wazi akaunti zake za mitandao ya kijamii facebook, twitter , instagram sambamba na kufungua TV ya Online itakayokwenda kwa jina la Kishki Online Tv.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa akaunti hizo, Shekh Kishk amesema kuwa jamii iliyokuwa inamfuatilia kwa kipindi kirefu walikuwa wanalalamika kwa kukosa mawaidha yake ambapo kwa kiasi kikubwa kinazidi kuwasogeza karibu nae.
“ Jamii inayonifuatilia ilikuwa inalalamika kila wakati wakisema kwanin Shekh haufungui mitandao ya kijamii na wengine walitaka kunifungulia ila sikuwa tayati, ila kuna baadhi ya watu walikuwa wanatumia mgongo wangu kufungua akaunti za facebook kwa kutumia jina langu na wakifanikiwa kwani walipata watu wengi kwa kipindi kifupi,”amesema Shekh Kishk.
Shekh Kishk amesema kuwa, katika akaunti hizo watu wataweza kupata darasa mbalimbali za hadithi, mawaidha, hotuba, hadithi na kutakuwa na usomaji wa Quran katika sauti saba, mbali na hilo kutakuwa na video za mawaidha na hotuba ambazo anazitoa wakati akiwa katika ziara za mikoani na hata nje ya nchi kwani amekuwa anatembea na watu wa habari kila mahala.
Amewatoa hofu watu kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii ndiyo inaweza kusababisha kufanya maovu ila ukiamua kuitumia vizuri inaweza kukuletea faida.
Kwa upande wa katibu wake anayejulikana kwa jina la Masawe, alisema kuwa kwa kipindi kirefu alikuwa anasumbuliwa na watu mbalimbali kwa nini Shekh Kishk hafungui akaunti za kijamii ila baad aya kukaa naye na kushauriana tukaamua kufungua na katika muda wa saa 24 ameweza kupata marafiki 5000 na kuamua kuwa na page ya facebook.
Shekhe Nurdeen Kishk akiwaonyesha waandishi wa habari jina analotumia katika mtandao wa kijamiiya facebook, twitter na instagram sambamba na Kishk Online Tv leo Jijini Dar es salaam.
Shekh Nurdeen Kishk akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kufungua akaunti za mitandao ya kijamii facebook, twitter na instagram sambamba na Kishk Online Tv zilizotambulishwa rasmi leo.
Katibu wa Shekh Nurdeen Kishk akizungumza na waandishi kuhusu namna jamii ilivyokuwa inatamani kuona Shekh anakuwa na akaunti katika mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment