Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Raia wa Denmark, Jesper Kirkanes wameandaa onesho la picha mbalimbali za maisha ya Watanzania zilizopigwa miaka 50 iliyopita.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Profesa Audax Mabula amesema onesho hilo ni muhimu kwa watanzania kujikumbusha maisha ya miaka 50 iliyopita.
Amesema kuwa onesho hilo litafanyika Novemba 16 katika viwanja vya makumbusho ya Taifa ambalo litafunguliwa na Balozi wa Denmark nchini, Einar Jensen.Profesa Mabula amesema kuwa katika siku ya onesho hilo hakutakuwa na kiingilio katika kuangalia picha hizo pamoja na picha zingine zilizomo katika makumbusho ya taifa.
Aidha amesema kuwa onesho la picha hizo ni pamoja maisha na kazi zilizokuwa zinafanywa watanzania ambapo kwa sasa watanzania wanatakiwa kujua historia ya maisha ya miaka 50 iliyopita.
Amesema wakati uliopo wa sera ya viwanda ni funzo kutoka kwa watanzania ambao waliishi kwa kuweza kuendesha maisha yao kwa kujitengenezea vitu ambavyo walikuwa wakihitaji.Profesa Mabula amesema kuwa picha hizo zilipigwa mwanzoni mwa mwaka 1968 mpaka mwaka 1977 na zilipigwa na Raia wa Denmark, Jesper Kirkanes ambaye alikuja nchini kwa kazi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa , Audax Mabula akizungumza na waandishi habari juu ya onesho la picha zilizopigwa miaka 50 iliyopita litakalofanyika Novemba 16 mwaka huu katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa.
Raia wa Denmark, Jesper Kirkanes ambaye alipiga picha za maisha ya watanzania miaka 50 iliypita akizungumza na waandishi habari juu ya maana picha hizo leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment