Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Vijijini ADLG iliyopo Jijini Mwanza, Jimmy Luhende akichangia mada kwenye Mkutano wa Sekta ya Uziduaji 2017 uliofanyika Mjini Dodoma.
Novemba 02-03, 2017 ulifanyika Mkutano wa Sekta ya Uziduaji (Madini, Mafuta na Gesi) Mjini Dodoma ambapo miongoni mwa maazimio kwenye mkutano huo ni Asasi za Kiraia kushiriki ipasavyo katika kuhakikisha Taifa linanufaika na Rasilimali zake.
Ungana na BMG kujua yaliyojiri kwenye mkutano huo ulioandaliwa na muungano wa Asasi za Kiraia zinazoangazia masuala ya Utawala Bora kwenye sekta ya Uziduaji nchini HakiRasilimali. Tazama HAPA ufunguzi wa mkutano huo. Tazama HAPA hafla ya usiku baada ya mkutano huo.Mwanasheria Veronica Zano (kushoto) kutoka Zimbabwe akichangia mada kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Vijijini ADLG iliyopo Jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment