Akizungumza leo Ijumaa Novemba 17,2017 wakati wa mkutano wa siku mbili uliohusisha nchi hizo tatu, meneja wa taasisi hiyo, Rosemary Mwaisaka amesema ili kutokomeza udumavu na magonjwa yasiyoambukizwa ni muhimu kuwekeza kwa watumishi wa afya wanaotoa huduma za kila siku kwenye vituo vya afya.
“Kwa kutambua hilo, tumetengeneza vitini kwa ajili ya watenda kazi katika ngazi ya vituo vya afya na jamii ili kutoa ujuzi katika masuala ya lishe, usalama wa chakula na kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa,” amesema Rosemary.
Amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi peke yao lakini lishe ni suala mtambuka.
Mwakilishi wa Wizara ya Afya nchini Kenya, Peter Cherotich amesema wamepokea vitini na kwamba, suala linalofanyiwa kazi sasa ni kuhakikisha usalama wa chakula na lishe unatiliwa mkazo.
Mwakilishi wa Wizara ya Afya nchini Kenya, Peter Cherotich amesema wamepokea vitini na kwamba, suala linalofanyiwa kazi sasa ni kuhakikisha usalama wa chakula na lishe unatiliwa mkazo.
No comments:
Post a Comment